Wiki iliyopita ya tarehe 8.8.2013, Apostle Gideon Mutalemwa aliakwa kuhudhuria na kuhudumu katika mkutano wa nje uliofanyika katika kanisa la HOPE FOR ALL NATION CHURCH MAFINGA IRINGA TANZANIA kwa Mchungaji Ambakisye.
Apostle Gideon Mutalemwa kutoka katika kanisa lake la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji kwa Nabii Flora Peter aliweza kumtuikia Mungu kwa njia ya uimbaji na kuhubiri Neno la Mungu. Watu walibarikiwa sana na huduma yake ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Apostle Gideon Mutalemwa ni mtu wa mkoa wa Bukoba lakini amekulia mkoa wa Iringa na wazazi wake wanaishi Iringa kwa muda mrefu sana. Mungu aliweza kumpa mke mwema kutoka mkoa huo wa Iringa na sasa ana mtoto mmoja wa kiume.
Ngoja tuone yaliyoajiri katika mkoa wa Iringa kwa njia ya picha:
KILIFIKA KIPINDI CHA KUMUIMBIA MUNGU
Apostle Gideon Mutalemwa akimwimbia Mungu katika mkutano wa nje mkoani Iringa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni