APOSTLE GIDEON HEADER ANIMATIONS

SHOOTING MPYA YA WIMBO WA MTAKATIFU WA MTUME GIDEON MUTALEMWA

Jumatano, 11 Septemba 2013

APOSTLE GISEON T. MUTALEMWA AFANYA MIKUTANO MIKUBWA MIWILI MKOA WA KAGERA MWEZI WA NANE NA MWEZI WA TISA 2013

Apostle Gideon T. Mutalemwa baada ya kufanya mikutano miwili mkoa wa Iringa, Mungu aliweza kumuwezesha na kupata kibali cha kufanya mikutano mingine miwili mkoa Kagera. Mungu amekuwa mwema sana kwa mtumishi wa Mungu kwa huduma anayofanya kwa juhudi zake akimtegemea Mungu kwa kila jambo. Watu wengi walikusanyika kusikiliza Neno la Mungu kwa kupitiia mtumishi Apostle Gideon Mutalemwa mkazi wa jiini Dar es Salaam. Watu waliofungwa na vifungo mbalimbali waliweza kufunguliwa na wengine kutamani kumgusa ili waweze kupata upako aliokuwa nao wakatii akihubiri injili.

Apostle Gideon T. Mutalemwa ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera na amekuwa akifanya kazi ya Mungu tangia utoto wake hapo mkoa Kagera chini ya Mchungaji Gerard Joseph. Katika ziara yake hii ya kumtumikia Mungu mkoani Kagera aliweza kubahatika kufanya huduma katika kanisa lake alilokulia kiroho linaloitwa Faith Mission ambalo bado linaongozwa na Mchungaji wake wa Kiroho, Gerard Joseph.

Watu walionekana kubarikiwa sana na huduma yake nyingine ya uimbaji. Kumbuka Apostle Gideon Mutalemwa mbali na kuhubiri pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili hapa Tanzania. Hivi karibuni aliweza kuzindua Albamu yake ya “SAMBAMBA NA YESU” jijini Dar es Salaam katika kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na mlezi wake wa kiroho  mtumishi wa Mungu Nabii Flora Peter.

Wakazi wa Kagera walionekana kuvutiiwa sana nabaadhi ya nyimbo za Kihaya ambazo mtumishi huyu mara nyingi hupenda sana kuziimba kwani amekuwa akifanya jitihada kuhakikisha Neno la Mungu linawafikia hata watu wasioweza kuelewa lugha ya Kiswahili. Amekuwa akiimba sana nyimbo za kiutamaduni na hii imemuwekea kuwa tofauti sana na waimbaji wengine. Ndani ya albamu yake hii kuna nyimbo za Kihaya kama  Tayesu wange na Mwaiyukage ambazo zimekuwa zikigusa mioyo ya walio wengi.

TUONE BAADHI YA MATUKIO YALIYOTOKEA MKOA WA KAGERA

WILAYA YA KARAGWE KAYANGA KAGERA

Apostle Gideon Mutalemwa akifanyiwa mahojiano  Radio na Karagwe Mtangazaji Katusi Tito

Mchungaji Jopec wa kanisala AGAPE Karagwe Kayanga Kagera
Apostle Gideon Mutalemwa
 Madiwani wa viti maalum wakicheza ngoma ya Kihaya

WILAYA YA MISSENYI KAGERA BUKOBA
 Apostle Gideon akiwa na bibi yake ambaye amemlea tangia utotoni
 Apostle Gideon akipata chakula kilichoandaliwa na bibi yale

Baada ya kupata mlo wa bibi kazi ya BWANA ilianza
 AKIHUBIRI KATIKA KANISALAKE LA KIROHO
Hapa ni kanisani kwa Apostle Gideon Mutalemwa. Mbali na kuwa kanisa pia palikuwa ni mahali pake pa kulala.  Aposle Gideon alisema kwa uchungu mkubwa sana alivyokumbuka kipindi anaishi Kagera na kulala kanisani kutokana na kukosa sehemu ya kulala. Chakula alikuwa akila kwa mchungaji wake na baadae anatandika kajigodoro madhabahunui na kulala....
 Apostle Dideon akilia kwa uchungu na kukumbuka maisha  ya hapo kanisani
Hapa alipokanyaga huyu dada ndipo alipokuwa akilala mtumishi wa Mungu Apostle Gideon Mutalemwa kipindi anaishi Kagera ..Akihubiri katika mitaa ambayo amekulia, alisema mitaa hii ilikuwa ni mitaa ya walevi....


....akiwa na bibi yake ambaye amemlea tangia utoto wake....