APOSTLE GIDEON HEADER ANIMATIONS

SHOOTING MPYA YA WIMBO WA MTAKATIFU WA MTUME GIDEON MUTALEMWA

Jumamosi, 17 Agosti 2013

APOSTLE GIDEON MUTALEMWA AACHA HISTORIA YA KIPEKEE KATIKA MKUTANO WA NJE-MAFINGA IRINGA

Wiki iliyopita ya tarehe 8.8.2013,  Apostle Gideon Mutalemwa aliakwa kuhudhuria na kuhudumu katika mkutano wa nje uliofanyika katika kanisa la HOPE FOR ALL NATION CHURCH MAFINGA IRINGA TANZANIA kwa Mchungaji Ambakisye.

Apostle Gideon Mutalemwa kutoka katika kanisa lake la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji kwa Nabii Flora Peter aliweza kumtuikia Mungu kwa njia ya uimbaji na kuhubiri Neno la Mungu. Watu walibarikiwa sana na huduma yake ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Hivi karibuni mtumishi wa Mungu huyu ameweza kutoa albamu yake ya "Sambamba na Yesu" ambayo imekuwa ikigusa sana mioyo ya watu hasa pale unaposikia ujumbe unaotolewa na mtumishi huyu wa Mungu. Uimbaji wake amejikita sana katika nyimbo za kiasili zenye kumtukuza Mungu na hasa zaidi kwa lugha ya Kihaya ambayo ndio lugha yake.

Apostle Gideon Mutalemwa ni mtu wa mkoa wa Bukoba lakini amekulia mkoa wa Iringa na  wazazi wake wanaishi Iringa kwa muda mrefu sana. Mungu aliweza kumpa mke mwema kutoka mkoa huo wa Iringa na sasa ana mtoto mmoja wa kiume.

Ngoja tuone yaliyoajiri katika mkoa wa Iringa kwa njia ya picha:

KILIFIKA KIPINDI CHA KUMUIMBIA MUNGU

 Apostle Gideon Mutalemwa akimwimbia Mungu katika mkutano wa nje mkoani Iringa











ULIFIKA WAKATI WA KUHUBIRI NENO LA MUNGU